Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu Wafanyabiashara sita kulipa faini ya Sh.Elfu 50 ama kwenda jela miezi 2 baada ya kukiri kosa la kuondoka nchini bila kufata utaratibu.
Hata hivyo ni washtakiwa watano ndio wamefanikiwa kulipa faini hiyo.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya Wakili wa Uhamiaji, Novatus Mlay kuwasomea mashtaka yao.
Washtakiwa hao wanadaiwa January 14, 2019 walikutwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakiwa wameondoka kwenda Afrika Kusini bila kuwa na vibali.
Baada ya kusomewa shtaka hilo, wastakiwa hao ambao wapo tisa, wawili walikana na sita walikiri kosa na kusomewa maelezo ya awali.
Katika maelezo ya awali, Wakili Mlay amedai January 14, 2019 washtakiwa walishushwa na ndege katika uwanja wa JNIA wakitokea Afrika Kusini ambapo walipelekwa Idara ya Uhamiaji Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano.
Wakili Mlay amedai katika maelezo ya onyo, washtakiwa walikiri kosa la kwenda Afrika Kusini bila Passport, ambapo walikamatwa kupitia Operation inayoendelea huko na kurudishwa nchini.


0 Comments